Magavana wakosoa msimamo wa Gachagua kuhusu fedha za kushughulikia athari za El Nino

  • | Citizen TV
    3,217 views

    Hali ya sintofahamu imeibuka kati ya Naibu Rais Rigathi Gachagua na baraza la magavana nchini kuhusiana na fedha za kukabiliana na athari za mvua ya el nino. Baraza la magavana likikanusha kupokea bilioni 10 kutoka kwa serikali kuu. Aidha naibu rais pia ameonekana kubadili msimamo wake wa awali kuhusu mgao wa bilioni kumi kwa kaunti kukabiliana na el nino.