Magavana wanasema hawajapokea mgao wao tangu Agosti

  • | Citizen TV
    1,445 views

    Baraza la magavana sasa limeonya kuwa shughuli katika kaunti zitalemazwa na kusitishwa hadi pale wizara ya fedha itakapotoa mgao wa kaunti. Katika kikao cha leo, magavana wamesema kuwa hawajapata pesa kuanzia mwezi Agosti hivyo malipo ya mishahara kwa wafanyikazi yamekuwa magumu. Hata hivyo waziri wa hazina john mbadi amekanusha matamshi ya magavana na kusema kuwa wizara ya fedha imetoa pesa za kaunti hadi Oktoba.