Magavana wataka serikali ingazie swala la mgao wa fedha kwa kaunti

  • | K24 Video
    37 views

    Baraza la magavana limeonya kuwa iwapo hawatapata mgao wa shilingi bilioni mia nne na hamsini, utoaji wa huduma kwa wananchi utakuwa tatizo katika kaunti mbalimbali huku madeni yakiongezeka. Kulingana na magavana ambao sasa wanalilia bunge la seneti kuwapa mgao huo, fedha nyingi zinatumiwa kulipa mishahara na marupurupu kwani kuongezeka kwa ushuru kama vile wa nyumba kunazidi kuongeza mzigo kwao wakisalia na fedha finyu kufanyia maendeleo. Macho yote sasa yanaelekezwa kwa kamati ya fedha ya seneti inayotarajiwa kutoa pendekezo la mgao kutoka kwa ushuru unaokusanywa kwa jumla nchini.