Magege ya wahalifu yavamia na kuwaibia wakazi Seme, Kisumu

  • | Citizen TV
    1,655 views

    Wakazi wa kijiji cha Alungo eneo la Seme Magharibi, kaunti ya Kisumu, wanaishi kwa hofu kutokana na mashambulizi yanayoenezwa na magenge ambayo yanachoma nyumba zao, baada ya kuitisha pesa na mali kutoka kwa wamiliki wa nyumba hizo. Watu wawili wemeuwawa huku maboma matatu yakiteketezwa. Na kama vile Seth Olale anavyotueleza, hakuna mshukiwa yeyote aliyekamatwa kufikia sasa.