Mahakama kuipatia tume ya EACC kibali cha kuzuia fedha za mpwa wa Ukur Yattani

  • | K24 Video
    57 views

    Mpwa wa aliyekuwa waziri wa fedha Ukur Yattani akiyepatikana na milioni sitini na mbili zikiwa kwa sarafu za dola sasa hatarejeshewa fedha hizo baada ya mahakama kuipea tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC kibali cha kuzuia fedha hizo kwa kipindi cha miezi sita. EACC inaamini kuwa huenda fedha hizo zilipatikana kwa njia ya ufisadi haswa ikizingatiwa alilipwa kwa njia tatanishi milioni sabini na moja na kaunti ya Marsabit katika kipindi ambacho yattani alihudumu kama gavana wa kwanza wa kaunti hiyo.