Mahakama Kuu Isiolo yampa afueni Gavana Abdi Guyo

  • | Citizen TV
    386 views

    Mahakama kuu ya Isiolo imesitisha kuondolewa ofisini kwa Gavana Abdi Guyo ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi aliyoiwasilisha. Jaji Heston Nyaga aliwazuia wawakilishi wadi wa Isiolo, kuendesha hoja ya kumng'atua Guyo ofisini iliyowasilishwa bungeni mnamo Juni 10. Wawakilishi wadi waliratibiwa kujadili hoja hiyo hapo kesho. Jaji pia aliagiza gavana apewe nakala ya notisi ya mashtaka, pamoja na nyaraka zote za msingi, ndani ya saa 48 za kutekelezwa kwa amri hiyo. Wana siku saba za kuwasilisha majibu yao.