Mahakama kuu yatarajiwa kuamua hatma ya sheria ya fedha mwaka elfu mbili ishirini na tatu

  • | Citizen TV
    1,434 views

    Mahakama kuu leo inaratajiwa kutoa mwelekeo kuhusu hatma ya sheria ya fedha mwaka elfu mbili ishirini na tatu kubaini endapo utekelezwaji wake utasitishwa au la. Wiki iliyopita mahakama hiyo iliongeza muda wa kusitisha utekelezaji wa sheria hiyo ya fedha hadi kesi iliyowasilishwa na seneta wa Busia Okiya Omtata na mbunge wa Rarieda Otiende Amolo imeskizwa. Upande wa serikali umetaka mahakama hiyo kutupilia mbali maagizo ya awali kupitia wakili prof. Githu Muigai ikilalama kuwa iwapo serikali itakosa kutekeleza sheria hiyo basi Kenya itajipata katika njia panda kwani haitaweza kukusanya ushuru inayonuia kutekeleza wajibu wake. Nao waliowasilisha kesi wakiwa na malalamishi kuwa tayari serikali kupitia shirika la udhibiti wa bei za kawi Epra imepuuza maagizo ya mahakama na kutekeleza baadhi ya mapendekezo yanayogusia sekta ya mafuta na kusababisha bei hiyo kupanda mno