Mahakama ya Meru yaamrisha kuwapunguzia kifungo wafungwa 11

  • | Citizen TV
    1,305 views

    Katibu Mkuu wa Idara ya Urekebishaji Tabia na Jela Nchini Salome Beaco ameongoza hafla ya kuzindua kiwanda cha kiufundi cha kuoka Mikate pamoja na ushonaji nguo, ambacho kimejengwa na Chandaria Foundation kama njia ya kupeana kwa jamii. Kwenye hotuba iliyosomwa na jaji mkuu wa Meru kwa niaba ya jaji mkuu wa Mahakama Nchi Martha Koome, Koome amesema uzinduzi huo ni ishara ya ushirikiano kati ya serikali na taasisi za binafsi kutatua changamoto katika jamii na taifa. Kama Njia ya kupunguza mrundiko katika jela ya Meru, mahakama ya Meru imetoa amri ya kuwapunguzia kifungo wafungwa 11 Ambao wataachiliwa huru.