Mahakama ya Wang'uru yapunguza dhamana kwa washukiwa wa wizi wa maandamano

  • | Citizen TV
    334 views

    Mahakama ya Wanguru hii leo imewapunguzia dhamana washukiwa kumi walioshtakiwa kwa makosa ya njama ya kushiriki wizi wakati wa maandamano, baada ya kumi hao kushindwa kulipa shilingi elfu hamsini kila mmoja. Wakati uo huo watu wengine watatu waliokabiliwa na mashtaka sawia kaunti ya Nyeri walikana mashtaka hayo yaliyojumlisha wizi kwenye duka la jumla la Naivas wakati wa maandamano ya saba saba.