Mahakama yaamuru Mackenzie na wenzake wafanyiwe uchunguzi wa kiakili

  • | K24 Video
    4 views

    Washukiwa 31 kati ya 94 wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji ya watu 429 walioaga dunia kutokana na itikadi kali, huko Shakahola, sasa watafanyiwa uchunguzi wa akili na kurudi mahakamani baada ya siku 20. Washukiwa hao walifikishwa katika mahakama kuu ya malindi, siku moja baada ya ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuridhishwa na uchunguzi uliofanywa na idara ya upelelezi wa jinai, DCI.