Mahakama yabatilisha ajira ya wafanyakazi wa bima ya SHA

  • | Citizen TV
    863 views

    Mahakama ya Ajira na Uhusiano wa Kazi imebatiliza zoezi la uajiri la Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) ikisema mchakato uliotumika si halali. Katika uamuzi uliotolewa Mei 29, 2025, Jaji Byram Ongaya aliamua kuwa ajira zilizofanywa na SHA hazikufuata Katiba na sheria, akitaja ukosefu wa uwazi, haki, na ushirikishwaji wa umma. Uamuzi huo ulifuatia ombi lililowasilishwa na mkenya Abdile, ambaye alidai kuwa SHA ilikiuka misingi ya utoaji wa huduma za kiutawala kuhusu haki na mchakato wa ajira wa ushindani katika zoezi hilo la kuajiri wafanyakazi.