- 958 viewsDuration: 2:38Inspekta jenerali wa polisi ndiye mwenye mamlaka ya kuwaajiri, kuwafuta na kuwahamisha maafisa wa polisi. Haya ni kwa mujibu wa mahakama ya leba ambayo ilitoa uamuzi huo kufuatia mgogoro kati ya Tume ya Kitaifa ya huduma za polisi NPSC - na idara ya polisi. Mahakama imesema kuwa NPSC haina mamlaka ya kuajiri maafisa wa polisi na kubatilisha tangazo la zoezi la usajili wa makurutu.
