Mahakama yazuia matangazo ya kesi ya Tundu Lissu

  • | BBC Swahili
    7,199 views
    Mahakama nchini Tanzania leo imezuia matangazo ya moja kwa moja na uchapishaji wa taarifa za mashahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kufuatia maagizo ya Mahakama Kuu ya kulinda mashahidi wa kiraia. Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franko Kiswaga, ameagiza upande wa mashtaka kurekebisha nyaraka za kesi ili kuficha utambulisho wa mashahidi. Je maamuzi haya yana maanisha nini kwa kesi inayomkabili Lissu?@RoncliffeOdit anachambua kwa kina suala hili kwa pamoja na taarifa nyingine nyingi saa tatu usiku wa leo, mubashara kwenye Dira ya Dunia TV kupitia ukurasa wa YouTube, BBC Swahili. - - #bbcswahili #kesi #tundulissu #tanzania #siasa #mahakama Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw