MAISHA NA AFYA - ATHARI ZA MAJANGA KATIKA AFYA YA BINADAMU

  • | VOA Swahili
    185 views
    Kulingana na Taasisi ya Afya ya Kitaifa ya Marekani, majanga asilia na yale yasababishwayo na binadamu huathiri mamilioni ya watu duniani kila mwaka. Wataalam wanashikilia kwamba majanga hayo yanaathiri afya ya umma moja kwa moja, yakiwemo majeraha ya mwili, magonjwa, na athari za kisaikolojia. Vile vile, majanga hayo yanaweza kuleta vifo, kuongeza kusambaa kwa magonjwa ya kuambukizwa, na kuharibu miundo mbinu, vituo vya afya vilijumuishwa. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.