MAISHA NA AFYA: Mfumo wa m-meng’enyo wa chakula na matatizo ya utumbo

  • | VOA Swahili
    120 views
    Mara nyingi tumbo linapofanya aina Fulani ya muungurumo, ni ishara ya kwamba unataka kupata haja kubwa. Lakini wakati mwingine, inaweza kuonyesha tatizo kubwa katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Watu wazima wanne kati ya kumi duniani wanakabiliwa na matatizo ya utumbo, kulingana na takwimu iliyochapishwa katika Jarida la Gastro-enter-ology. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unajumuisha njia ya utumbo au njia ya GI, tumbo, utumbo mdogo na mkubwa, pamoja na viungo vya ndani ya mwili kama ini, kongosho, na nyongo. Inasaga chakula ili kupata uwezo wa kunyonya maji na kutoa virutubisho, madini, na vitamini kwa ajili ya matumizi ya mwili, huku pia ikiondoa taka mwilini.