- 2,242 viewsDuration: 5:40Mariam Ali, msichana wa Kitanzania mwenye miaka 26, ambaye miaka miwili baada ya kuhitimu Shahada ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aligundulika kuwa na ugonjwa wa figo. Leo, Mariam anafanya kazi za usafi majumbani kujisitiri na kukusanya fedha za matibabu kitaalamu dialysis na hatimaye kupandikiza figo ili kuokoa maisha yake. Hivi karibuni wataalamu wa figo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wameonya kuhusu ongezeko la ugonjwa sugu wa figo kwa vijana walio chini ya miaka 50 nchini Tanzania. Je, Mariam alipokeaje taarifa hiyo? Na ni maswali gani yalijaa kichwani mwake kuhusu hatma ya maisha yake? Martha Saranga amezungumza nae katika WARIDI WA BBC. #bbcswahili #tanzania #waridiwabbc Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw