- 985 viewsDuration: 2:57Idadi ya watu waliofariki kufuatia maporomoko ya ardhi eneo la Elgeyo Marakwet sasa imefikia 32. Hii ni baada ya maiti 4 kupatikana eneo la Chesongoch na watu wengine wawili kufariki katika maporomoko mengine ya ardhi kijiji cha Kipkenda eneo bunge la Keiyo North. Miongoni mwa waliofariki na maporomoko haya ni wanafunzi 14.