Majaji watatu wa Mahakama Kuu kusikiza kesi kuhusu sheria ya fedha

  • | Citizen TV
    1,410 views

    Kesi yakupinga utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya Mwaka wa 2023 inatarajiwa kuanza kuskizwa hapo kesho na majaji watatu walioteuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome. Jaji David Majanja ataongoza Majaji Christine Meoli na Lawrence Mugambi kuskiza kesi hiyo iliyokuwa mbele ya Jaji Mugure Thande na ambaye alipendekeza kuskizwa kwa kesi hiyo na zaidi ya jaji mmoja akisema inaibuwa masuala ya kikatiba.