Majambazi wamuua polisi wa akiba na kuiba bunduki yake Baringo

  • | Citizen TV
    537 views

    Wezi wa mifugo wamemuua na kutwaa bunduki ya afisa wa akiba eneo la Nosukuro kaunti ya Baringo watu wengine wawili akiwemo naibu mwalimu mkuu wa shule ya Nosukuro wanauguza majeraha baada ya kupigwa risasi na majambazi hao. Mwendazake ambaye alikuwa anasindikiza mwalimu huyo pamoja na mwendeshaji wa boda boda alipigwa risasi kifuani na kufariki papo hapo. Wakazi wanaitaka serikali kufanya operesheni ya kukomesha mauaji ya kiholela eneo hilo.