- 12,296 viewsDuration: 2:53Wakazi wa eneo la Mundika viungani mwa mji wa Busia wanahofia usalama wao baada ya mhudumu wa duka la Mpesa kuuwawa na majambazi katika duka lake siku ya Jumatatu. Mwendazake alipigwa risasi nje ya duka lake wakati wa mchana, kabla ya majambazi hao kufyatua risasi kiholela kuwafurusha wafanyabiashara na wananchi kwenye soko hilo na kutoweka na shilingi elfu mia nane. Majambazi hao wawili waliokuwa na bunduki aina ya AK 47 na pikipiki isiyokuwa na nambari ya usajili walitoweka muda mfupi baada ya tukio hilo ikiaminika waliingia taifa jirani la Uganda kupitia njia za mkato. Wananchi na viongozi wenye ghadhabu wameshutumu vikali kisa hicho wakiwasuta maafisa wa usalama kwa kuzembea kazini. Aidha, wakazi hao wa Mundika wamesisitiza kuwa maafisa wa polisi wa kambi za Esikulu na Mabatini Korinda wanapaswa kupewa uhamisho wa lazima kwani usalama umedorora pakubwa katika siku za hivi karibuni..