- 8,383 viewsDuration: 3:21Majibizano yamechacha kuhusiana na fujo zilizoshuhudiwa Ijumaa wakati wa mkutano wa chama cha DCP katika Kaunti ya Nakuru. Viongozi wa serikali na upinzani wanalaumiana kuhusu waliopanga vurugu katika eneo la Soko Mjinga, huku Kinara wa DCP Rigathi Gachagua akidai kuwa baadhi ya viongozi serikalini walipanga na kufadhili ghasia hizo. Haya yanajiri huku Katibu wa Usalama Raymond Omollo akitoa hakikisho kuhusu ulinzi wa viongozi wote bila ubaguzi.