Majimbo mengi zaidi yafanya uchaguzi wa awali siku ya Super Tuesday

  • | VOA Swahili
    167 views
    Majimbo mengi zaidi yatafanya uchaguzi wa awali, Machi 5, kuliko siku yoyote nyingine katika kipindi cha uchaguzi huu. Ndio maana inaitwa Super Tuesday. Majimbo kumi na tano na mkoa mmoja utapiga kura siku ya Super Tuesday mwaka huu. Huko Iowa, matokeo ya uchaguzi wa awali wa Wademokratiki utatangazwa. Inahitajika wajumbe waliochukua ahadi 1,968 – asilimia 50 ya wajumbe wote – kushinda uteuzi wa mgombea urais wa Chama cha Demokratiki. Inahitajika wajumbe 1,215 – asilimia 50 ya wajumbe wote – kushinda uteuzi wa mgombea urais wa Chama cha Republikan. Msemo Super Tuesday haukuanza kujitokeza hadi mwaka 1976. Bill Clinton alipata uungwaji mkono kutokana na ukakamavu wake wa kujitokeza siku ya Super Tuesday mwaka 1992 katika safari yake kuelekea White House. #supertuesday #uchaguzimkuu #marekani #majimbo #iowa #uchaguziwaawali #voa #voaswahili ⁣