Makaburi mengine manne na mafuvu yapatikana Binzaro

  • | Citizen TV
    1,974 views

    Makaburi mengine manne yamepatikana katika kijiji cha Binzaro, kaunti ya Kilifi. Matukio hayo yamezua taharuki huku polisi na wakazi wakihofia kuwa huenda wafuasi zaidi wa dhehebu potovu katika eneo hilo wamefariki. Wizara ya usalama inasema kuwa imetibua kuenea kwa dhehebu hilo ambalo linakisiwa kuandamana na mafunzo ya itikadi kali kama ilivyoshuhudiwa katika msitu wa Shakahola miaka miwili iliyopita.