Makadinali 133 wajumuika mjini Vatican kumchagua papa mpya

  • | Citizen TV
    3,805 views

    Jumla ya Makadinali 133 tayari wamejumuika katika kanisa maalum la Sistine, mjini Vatican, kuanza rasmi shughuli ya kumchagua Papa mpya atakayeongoza kanisa Katoliki duniani. Shughuli ya kumchagua mrithi wa Papa marehemu Francis inaanza kesho Jumatano, huku zaidi ya waumini elfu ishirini wakisubiri kutangazwa kwa Papa Mpya kupitia kwa Moshi mweupe, katika eneo la St Peter's Square, kama Seth Olale anavyotuarifu