Makadirio kuziba mianya katika bajeti I Kamati ya bajeti kushirikisha umma hivi karibun

  • | KBC Video
    71 views

    Kamati ya Bunge la taifa kuhusu Bajeti na makadirio ina chini ya siku 10 kufanya shughuli ya ushirikishi wa umma kwenye makadirio ya bajeti ya ziada ya mwaka wa fedha wa 2024/25 kama ilivyotakiwa na Hazina ya Kitaifa. Spika wa bunge la taifa Moses Wetangula siku ya ijumaa aliagiza kamati hiyo kuzingatia makadirio hayo na kuwashirikisha wananchi kabla ya kuwasilisha ripoti yake bungeni ifikiapo tarehe 24 mwezi huu ambapo bunge litarejelea vikao vyake kutoka likizoni. Makadirio hayo yanawadia baada ya kutupiliwa mbali kwa mswada wa fedha wa mwaka wa 2024. Hii ilisababisha kupunguzwa kwa shilingi bilioni 1.8 kutoka kwa bajeti hiyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive