Makala ya Batuk, Mabinti na Haki

  • | Citizen TV
    1,877 views

    Ni miezi sita sasa tangu bunge la taifa kuanzisha uchunguzi dhidi ya visa vya uhalifu vinavyodaiwa kutekelezwa na wanajeshi kutoka Uingereza ambao wanafanya mazoezi katika kambi ya kijeshi ya BATUK, kaunti za Samburu na Laikipia. Madai hayo yanahusu mauaji, unyanyasaji wa kijinsia na kuwaacha watoto wachanga waliozaliwa kutokana na dhulma hizo bila msaada wowote. Balozi ya Uingereza nchini amesema kwamba anashirikiana na vitengo mbalimbali vya uchunguzi nchini ili kufanikisha na kukamilisha uchunguzi kuhusiana na madai ya uhalifu yaliyoendelezwa na wanajeshi wa BATUK. Seth Olale anasimulia madhila hayo kwenye awamu ya kwanza ya Makala ya BATUK, MABINTI NA HAKI.