Makamishna wapya wa IEBC waapishwa

  • | KBC Video
    271 views

    Mwenyekiti mpya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka -IEBC, Erastus Edung ameahidi kutekeleza wajibu wake kwa kujitolea na kulinda haki za kidemokrasia za Wakenya kwenye uchaguzi mkuu ujao. Akiongea kwenye majengo ya mahakama ya upeo muda mfupi baada yake na makamishna wengine sita kuapishwa, Edung alisema chaguzi huru na za kuaminika ni msingi wa demokrasia inayonawiri, na maafisa wa tume hiyo watajikakamua kuafikia lengo hilo kwa uaminifu. Jaji mkuu Martha Koome, aliyeongoza hafla hiyo aliwatahadharisha makamishna hao wapya kwamba walikuwa wanaingia afisini wakati ambapo wakenya tayari wameeleza kutoridhishwa na utendakazi wa taasisi za umma.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News