Makanisa ya kiinjilisti yaandaa maombi kwa taifa Nairobi

  • | Citizen TV
    336 views

    Baraza la Kitaifa la Makanisa ya kiinjilisti liliongoza ibada ya maombi ya pamoja kwa ajili ya amani, kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika Juni 25. Mkutano huo uliwaleta pamoja viongozi wa makanisa, vijana na familia zilizopoteza wapendwa wao wakati wa maandamano ya mwaka jana. Wito wa haki na uponyaji ulishamiri katika ibada hiyo iliyolenga kuunganisha taifa kupitia maombi na tafakari, huku vijana wakihimizwa kuepuka vurugu na fujo katika maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu maandamano ya Gen Z.