Makanisa yataka sheria ibuniwe ya kudhibiti imani potovu

  • | Citizen TV
    133 views

    Baadhi ya makasisi kutoka makanisa ya kiinjilisti sasa wanashinikiza kuundwa kwa bodi maalum itakaoyowaleta Pamoja wahusika wakuu kutoka serikali na makanisa hapa nchini ili kutoa mwelekeo dhabiti wa utendakazi. Kwa mujibu wa mkutano wa makasisi hapa jijini Nairobi, wapo baadhi yao ambao wameweka mbele imani potovu, wakisisitiza ni lazima serikali iingilie kati ili kuwanusuru wakenya ambao wanaingia katika mitego yao