Skip to main content
Skip to main content

Makelele yazuka wakati wa hotuba ya Trump

  • | BBC Swahili
    16,470 views
    Duration: 52s
    Rais wa Marekani Donald Trump amekosolewa kwa sauti na kelele alipokuwa akitoa hotuba ya Hali ya Taifa. Wakati Warepublican wakimpa Trump shangwe za kusimama alipokuwa akizungumzia sera yake ya uhamiaji, aliwakemea wale ambao hawakusimama akisema, “Mnapaswa kuwa na aibu.” Tukio hilo la mvutano lilitokea wakati Trump alipowahimiza wabunge kuunga mkono msimamo wa serikali ya Marekani wa kutoa kipau,bele kwa kulinda raia wa Marekani kwanza kuliko raia wa kigeni. Baadhi ya wabunge wa chama cha Democratic, akiwemo Ilhan Omar na Rashida Tlaib, walimpigia kelele wakionyesha kutokubaliana naye. - - #bbcswahili #trump #wahamiaji #marekani🇺🇸 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw