MAKOVU YA JUNI 2024: Baadhi ya waathiriwa wasalia na risasi mwilini

  • | Citizen TV
    1,582 views

    Ni mwaka mmoja baada ya maandamano ya Gen Z yaliyotikisa taifa na kusababisha mauaji na majeraha kwa baadhi ya vijana nchini. Japo kuna wale waliotibiwa na kuendelea na maisha yao, kuna wengine ambao maisha yao yalibadilika kabisa. Samuel Kinyanjui na Rogers Mwabe wamesalia na makovu ya milele, baada ya kulengwa na risasi wakati ya maandamano hayo ya mwaka jana.