Makumi ya waandamanaji wamekamatwa na polisi nchini Uganda

  • | Citizen TV
    6,045 views

    Katika taifa jirani la Uganda, polisi mjini Kampala wamewakamata watu kadhaa waliokuwa wakiandamana kuelekea bungeni kuwasilisha malalamishi dhidi ya maafisa wa umma waandamanaji hao wameonekana kuiga mkondo wa maandamano ya humu nchini yaliyoanzishwa na vijana wa Gen Z huku wao wakimtaka spika wa bunge la Uganda Annet Among kujiuzulu pamoja na makamishna wanne wa tume ya uchaguzi. Awali Rais Yoweri Museveni aliwaonya waandamanaji kwamba watakabiliwa vilivyo iwapo wataandamana