Makundi ya kigaidi yanatumia teknolojia ya kisasa kuwavutia vijana na watoto kujiunga nao

  • | Citizen TV
    583 views

    Ripoti ya serikali kuhusu tishio la mashambulizi ya kigaidi nchini imebaini kuwa makundi ya kigaidi yanatumia mbinu mpya za teknolojia ya kisasa na sarafu za kidijitali au cryptocurrency, kuwavutia vijana na watoto kujiunga na makundi hayo. Akizungumza katika kongamano lililoleta pamoja mataifa kumi na tano barani afrika, mshauri wa maswala ya usalama katika afisi ya rais monica juma ,sasa anawataka wananchi kushirikiana na serikali kufunga mianya ya ufadhili wa aina yoyote wa ugaidi nchini.