Makundi ya wanawake mombasa yapewa mashine za kutengeneza mafuta ya nazi

  • | Citizen TV
    236 views

    Makundi ya wanawake kaunti ya Mombasa yamepigwa jeki kwa kupewa mashine za kutengeneza mafuta ya nazi. Mradi huo uliofadhiliwa na ubalozi wa Uturuki nchini kwa ushirikiano wakfu wa ushiriki wema unaongozwa na mkewe mkuu wa mawaziri Tessie Musalia, unalenga kuwanufaisha wanawake kibiashara. Akiongea huko shanzu mombasa wakati wa kutoa mashine hizo, mkewe mudavadi ametaka wanawake nchini kujitokeza na kumiliki biashara ili kuchangia katika uchumi pamoja na kupiga teke uchochole katika jamii za pwani.