Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa yateketea baada ya soko la Shauri mjini Embu kushika moto

  • | K24 Video
    36 views

    Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa imeteketea baada ya soko la Shauri mjini Embu kushika moto. Kulingana na waliokuwa hapo, chanzo cha moto kinadaiwa kuwa bomu la kutoa machozi lililorushwa na maafisa wa polisi katika karakana moja iliyoko karibu. Tukio hilo linasemekana kujiri, wakati maafisa wa usalama walipokuwa wakidhibiti maandamano ya waendeshaji boda boda.