Malori yaliobeba msaada yakisubiri katika mpaka wa Misri na Israel

  • | VOA Swahili
    717 views
    Magari, yanayoelezewa ni malori yaliobeba misaada ya Taasisi ya Sinai ya Haki za Binadamu, yalionekana yamejipanga mstari katika mpaka wa Misri na Israel karibu na kivuko cha mpakani cha Nitzana katika kanda ya video iliyosambazwa katika mitandao yao ya kijamii Jumatatu (Februari 12). Shirika la Habari la Reuters liliweza kuthibitisha eneo hilo ni karibu na kivuko cha mpakani cha Nitzana huko Misri. Sehemu za majumba, bara na magorofa zinalingana na picha za satellite za eneo hilo. Reuters haikuweza yenyewe kuthibitisha tarehe ambayo kanda hiyo ya video ilichukuliwa. Israel imekanusha kuzuia msaada, wakati Misri huko siku za nyuma ilisema kuwa “vikwazo vya Israeli” ikwemo utaratibu wa kuyakagua malori yalikuwa yanachelewesha ufikishaji wa misaada kwa haraka ndani ya Ukanda wa Gaza. Shambulizi la Israel dhidi ya Hamas limewaacha zaidi ya watu milioni 2.3 huko Gaza bila makazi na wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula, maji, madawa na mafuta. Mashambulizi haya yalianza Oktoba 7 kufuatia mauaji ya Oktoba 7 huko kusini mwa Israel, yaliofanywa na wanamgambo kutoka Gaza waliouwa takriban watu 1,200 na kuwateka watu 250. ⁣⁣ - Reuters #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran