Mamia ya wanafunzi walazimika kurejea nyumbani

  • | Citizen TV
    6,929 views

    Mamia ya Wanafunzi wamekwama katika vituo tofauti vya magari ya usafiri wa umma katika maeneo tofauti nchini, baada ya wizara ya elimu kuahirisha ghafla ufunguzi wa shule usiku wa manane. Taarifa hiyo ya wizara iliahirisha Ufunguzi wa shule kwa wiki moja kufuatia mafuriko yanayoshuhudiwa sehemu kadhaa za nchi. Uamuzi huo ukiwaghadhabisha wazazi wengi waliolalamikia kwanini ujumbe huo haungetolewa mapema kabla ya wanafunzi kuanza safari.