Mamilioni ya watu wavutiwa na tukio la kupatwa kwa jua

  • | VOA Swahili
    546 views
    Wakazi wa Marekani wameshuhudia tukio kubwa la kupatwa kwa jua Aprili Nane. Inakadiriwa kuwa watu milioni 32 wanaishi ndani ya njia maalum ambayo mwezi ulilizuia kabisa jua na wakazi wengine milioni 150 wanaoishi chini ya maili 200 (kilomita 320) kutoka ukanda huo, haya ni kwa mujibu wa NASA. Wafanyabiashara wengi walijitokeza kwa matukio maalum na huko Cleveland, ambapo viongozi wa eneo hilo wanatarajia wageni 200,000, Rock & Roll Hall of Fame inapanga "Solarfest" ya siku nne ya muziki wa moja kwa moja. Perryman Group, kampuni ya utafiti yenye makao yake makuu Texas, ilikadiria athari za kiuchumi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kutokana na tukio la kupatwa kwa jua kwa mwaka 2024 na inaweza kufikia dola bilioni 6. Mwaka huu watu wanaoishi katika njia maalum yenye upana wa maili 115, pana zaidi kuliko mwaka 2017. Inaanzia magharibi mwa Mexico, kupanda juu. kupitia miji ya Marekani ya Dallas, Indianapolis, na Buffalo, kabla ya kuishia mashariki mwa Canada. Shule nyingi zilizo kwenye njia maalum zitafungwa au kuwaruhusu wanafunzi kutoka mapema, pamoja na huko Cleveland na Montreal. #northamerica #us #mexico #canada #total #solar #eclipse #voaswahili #voa #nasa #NASA #NOAA #jua #mwezi #kupatwa #marekani