Manyanyaso dhidi ya wanawake yameongezeka wakati wa janga la Corona, Je tufanye nini kuyapunguza?

  • | BBC Swahili
    Hujambo? Karibu katika AMKA NA BBC, kwa muktasari tuliyonayo ni pamoja na ;- Umoja wa Mataifa waelezea wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Ethiopia na kutaka kuwepo kwa huru wa watu kutoka na kuingia jimboni Tigray. Wakazi wa Kunduchi Mtongani Jijini Dar es Salaam wameshauriwa kuhama maeno yao baada ya kutokea kwa hali ya kijiolojia inayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama Liquefaction. Serikali ya DRC yakiri kwamba mwanasiasa mkongwe anayetumikia kifungo cha miaka 20 jela Vital Kamere ni mgonjwa na huenda akahitaji matibabu nje ya nchi. Na leo ni siku ya umoja wa mataifa kupinga unyanyasaji wa wanawake duniani, takwimu zaonyesha manyanyaso kuongezeka katika baadhi ya nchi haswa wakati wa janga la Corona, katika gumzo tunauliza nini kifanyike kupunguza manyanyaso haya? utakuwa nami Regina Mziwanda na michezoni utakuwa na David Nkya AMKA NA BBC