Maombi maalum ya kuombea amani msimu wa kampeni

  • | K24 Video
    49 views

    Kama njia moja ya kudumisha amani katika mpaka wa kaunti za Kiambu na Narok,ambapo kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano kutokana na wizi wa mifugo,idara ya usalama,kanisa,viongozi wa jamii zote mbili pamoja na wakaazi wa kaunti hizo,sasa wameandaa maombi maalum,lengo kuu likiwa ni kuombea amani, huku pia wakijadili jinsi jamii hizo mbili zitaendeleza amani msimu huu wa kampeni.