Mapacha wa Brazil watenganishwa baada ya operesheni saba

  • | BBC Swahili
    999 views
    Mapacha ambao walikuwa wameungana kichwani walitenganishwa kwa ufanisi kwa msaada wa picha halisi (virtual reality ) kutoka kwa madaktari wa nchi nyingine. Upasuaji wa watoto Bernardo na Arthur Lima wenye umri wa miaka 3, ulifanyika Rio de Janeiro. Kwa miezi kadhaa, timu za madakrati wa upasuaji zilijaribu aina tofauti za mbinu kwa kutumia picha za mapacha hao katika teknolojia ya picha ambayo ilitegemea uchunguzi wa CT na MRI. #bbcswahili #afya #brazil