Mapato ya misitu ya mikoko Lamu

  • | Citizen TV
    1,814 views

    Ardhi chepechepe, ina umuhimu sana wa kukuza misitu ya mikoko hasa katika maeneo ya Pwani. Mikoko hunawiri katika mazingira kama hayo. Kundi moja katika kisiwa cha Patte kaunti ya Lamu kinatumia misitu ya mikoko kujichumia riziki bali na kukuza utalii pamoja na kutunza mazingira. Mwanahabari wetu Agnes Oloo amerejea kutoka Patte na Taarifa ifuatayo.