Mapendekezo ya kubadili sera za HELB yapingwa

  • | K24 Video
    2 views

    Bodi ya kutoa mikopo ya elimu ya juu HELB imepinga vikali mapendekezo ya kupunguza muda na riba ya mikopo inayotoa. Mapendekezo hayo yaliyo katika mswada wa helb mwaka wa 2023 uliotayarishwa na mbunge wa Machakos Joyce Kamene, unalenga kurekebisha na kupunguza kiwango cha riba kutoka asilimia 4 hadi 3 huku watu wakipewa nafasi ya miaka mitano kabla ya kuanza kulipa mikopo hiyo. Haya yanajiri wakati serikali bado haijawasilisha ufadhili na mikopo kwa wanafunzi waliopata nafasi katika vyuo vikuu