Mapendekezo yakuwapa fursa wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi

  • | K24 Video
    34 views

    Mashirika yasiyo ya kiserikali likiwemo la Crawn trust linaloongozwa na Daisy Amdany, yametoa mapendekezo ambayo yatahakikisha idadi ya thuluthi moja ya jinsia ya kike katika mabunge ya taifa na seneti itaafikiwa. Mashirika hayo yamewataka wabunge kulipa uzito suala hilo ili kuwapa fursa wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi. Akizungumza katika kongamano lililowaleta pamoja wadau wa masuala ya uongozi wa mwanamke nchini, mshauri wa ofisi ya rais wa masuala ya haki za wanawake Harriet Chiggai amesema serikali ya kenya kwanza inapania kutekeleza sheria ya uwakilishi wa jinsia kikamilifu.