Maporomoko ya 14-falls ‘yadidimia’

  • | NTV Video
    769 views

    Eneo la Kivutio cha watalii la maporomoko ya maji ya Fourteen Falls eneo la Thika katika kaunti ya Kiambu, liko katika hali ya kutokomea kufuatia mafuriko ya hivi maajuzi. Eneo hili lilitambulika na watalii wa kigeni pamoja na wenyeji waliofika hapo ili kufurahia mandhari nzuri na utulivu wake. Hata hivyo, uchafuzi mkubwa wa Mto Athi, ambao ndio uti wake, pamoja na maji taka na uchafu wa viwandani umefanya eneo lililokuwa likitembelewa sana kuachwa tupu. Kwa sasa, rundo la takataka zilizosombwa kutoka Nairobi na viunga vyake tayari linasakama eneo hilo. Wakizungumza wakati wa kusafisha 14-falls, washikadau walikiri kuwa maji hayo machafu yameharibu shughuli nyingi za kiuchumi kwenye mto huo ikiwemo uvuvi na kilimo.

    Subscribe to NTV Kenya channel for latest Kenyan news today and everyday. Get the Kenya news updates, discussions and other exciting shows.

    Website: ntv.nation.co.ke || Paper: Daily Nation || Twitter: @ntvkenya || Facebook: NTV Kenya || Instagram: NTV Kenya