- 25,336 viewsDuration: 34sPentagon imesema kwamba itatekeleza hukumu ya kifo kwa aliyekuwa Meja wa Jeshi la Marekani kwa kupigwa risasi na kikosi maalumu cha wapiga risasi. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa jeshi la Marekani kutekeleza hukumu ya aina hiyo tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia. Nidal Hasan, aliyekuwa daktari wa magonjwa ya akili katika Jeshi la Marekani, aliwapiga risasi wanajeshi 13 wasio na silaha na kuwaua katika kituo cha kijeshi cha Fort Hood mwaka 2009 na wengine 32 walijeruhiwa. Utekelezaji wa hukumu hiyo umepangwa kufanyika tarehe 3 Desemba #bbcswahili #marekani #haki Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw