- 21,022 viewsDuration: 30sMajeshi ya Marekani yamekamata meli ya mizigo yenye bendera ya Iran katika Ghuba, kama sehemu ya kizuizi chake cha kijeshi cha baharini, amesema rais wa Marekani Donald Trump. Rais huyo aliandika kwenye mtandao wake wa Truth Social kwamba meli hiyo, inayoitwa Touska, ilikamatwa na Jeshi la majini la Marekani baada ya kushindwa kufuata onyo la kusimama. Iran imesema kuwa kitendo hicho ni ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano na kwamba italipiza kisasi hivi karibuni kwa kile ilichokiita “kitendo cha uharamia wa kijeshi. #bbcswahili #marekani #iran Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw