Marekebisho ya Kalenda ya masomo yatangazwa

  • | KBC Video
    26 views

    Tarehe za likizo fupi kwa wanafunzi wa shule za umma zimesongezwa mbele hadi tarehe 26 mwezi Juni kutoka tarehe 20 mwezi Juni, kufuatia marekebisho ya kalenda ya masomo na wizara ya elimu. Katika arifa ya katibu wa elimu ya msingi Belio Kipsang kwa wakurugenzi wote wa elimu katika Kaunti, Kipsang anasema uamuzi huo ulitokana na kuahirishwa kwa tarehe za kufungua shule. Kufuatia mabadiliko hayo, wanafunzi wa shule za chekechea, msingi na sekondari watakuwa na likizo fupi kwa siku 3 kuanzia Jumatano tarehe 26 mwezi Juni hadi Ijumaa tarehe 28 mwezi Juni.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive