Mariakani police officer helps boy in Kaloleni, Kilifi

 • | Nation Video
  5,781 views

  Heri tendo moja jema kuliko mamilioni ya nia njema.

  Hivi ndivyo wavyele walivyosema.

  Kutana na askari polisi Edward Akoko kutoka kituo cha polisi Mariakani.

  Akoko alitawala kwenye mtandao wiki iliyopita baada ya kumtunuku kijana George na viatu aina ya ‘slippers’

  George Charo Ngowa kijana mwenye umri wa miaka kumi na mitano anasomea shule ya msingi ya Minyenzeni huko Mariakani kata ndogo ya Kaloleni,Kilifi Kaunti.

  Kama kawaida yake akielekea shule miguu chuma,Afisaa Akoko alimuita na kumshauri amuone anaporudi nyumbani kwa chamcha.

  Kama kawaida polisi anapokuita na si mazoea basi mtu huwa na hofu.

  Pindi tu muda ulipofika,akiwa na wenzake wakielekea nyumbani huku akihofia alishurutishwa na wenzake wapiti karibu na huyo afisaa.

  Shingo upande George alijipeleke hapo ndio akatunukiwa viatu vya champali.

  Kulingana na mamake,Jumwa Ngala,hakutarajia mtoto wake kuja nyumbani na viatu bipya na alidhania huenda akawa ameiba hivyo basi akaanza kumdadisi.

  Hakutosheka na maelezo yake hadi alipouliza marafiki zake ndio roho ikamtulia akaamini kwamba alipewa viatu hivyo na askari polisi.

  Ni nadra sana katika jamii kuona askari kama huyu akijinyima ili kuona kwamba kijana anaonekana nadhifu.

  Katika mahojiano na afisaa huyo,aliele