Martha Karua afurushwa Tanzania

  • | Citizen TV
    6,001 views

    Kiongozi Wa Chama Cha People's Liberation Party, Martha Karua, Mtetezi Wa Haki Za Binadamu Lynn Ngugi, Na Mwanachama Wa Baraza La Lsk Gloria Kimani Hatimaye Wamerejea Nchini Baada Ya Kuzuiliwa Nchini Tanzania Kwa Takriban Saa Sita. Watatu Hao Walifurushwa Tanzania Baada Ya Kutua Katika Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Wa Mwalimu Nyerere, Mjini Dar Es Salaam. Na Kama Anavyoarifu Ben Kirui, Karua Anasema Kuwa Walikuwa Wamesafiri Tanzania Kwa Mwaliko Wa Jumuiya Ya Wanasheria Wa Afrika Mashariki Kuhudhuria Kesi Dhidi Ya Kiongozi Wa Upinzani Tundu Lissu Ambaye Ameshtakiwa Kwa Uhaini.